• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bingwa wa zamani wa ndondi Jake LaMotta afariki dunia

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:39:27

    Bingwa wa zamani wadunia wa Marekani wa uzito wa kati na mchekeshaji, Jake LaMotta amefariki dunia Septemba 19 mwaka huu akiwa na umri wa 95. LaMotta ambaye alitamba zaidi katika tasnia ya mchezo wa ngumi kuanzia miaka ya 1949 hadi 1951 amefariki nyumbani kwake kutokana na tatizo la homa ya mapafu.

    LaMotta ambaye alizaliwa Julai 10 mwaka 1922 atakumbukwa kwa uvaaji wa kaptula yenye mistari ya chuichui na wakati fulani alikua akiingiza uchekeshaji wakati akipigana jambo lililomfanya mpinzani wake kuishia kucheka na yeye kushinda.

    LaMotta alipata ubingwa wa dunia wa uzito wa kati June mwaka 1949 wakati alipokabiliana na mfaransa, Marcel Cerdan na kumpiga katika raundi ya 10 ya pambano. Bingwa huyo amepigana jumla ya mapambano 106 katika miaka 13 ya tasnia yake ya ngumi, akishinda mara 83 na kutoka sare mara 4 pamoja na kupigwa mapambano 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako