• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid yabanjuliwa 1-0 na Real Betis

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:39:53

    Juzi usiku klabu ya Real Madrid ilirudi katika uwanja wake wa Santiago Bernabeu kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Real Betis, Madrid walirudi wakiwa na nyota wao Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa amefungiwa game nne na LaLiga. Real Betis wamefanikiwa kuondoka na point tatu Santiago Bernabeu baada ya kuifunga Real Madrid goli 1-0, goli la Real Betis likifungwa dakika ya 90 na Sanabria Ayala, kipigo hicho kinavunja rekodi mbili za Real Madrid ambapo michezo hiyo ndio inakuwa ya kwanza kumalizika na Real Madrid kutofunga goli toka April 2016 dhidi ya ManCity (0-0). Real Madrid pia wanashindwa kuendeleza rekodi yao ya kupata ushindi katika michezo 73 mfululizo, rekodi ambayo ilidumu kwa miaka baada ya kuwekwa na club ya Santos mwaka 1963, Real Madrid wameifikia rekodi hiyo ya Santos lakini wameshindwa kuivunja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako