• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania wafanya vizuri na timu zao

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:40:23

    Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania mshambuliaji Mbwana Samatta, Simon Msuva na Abdi Banda wamefanya vizuri kwenye vilabu vyao katika michezo ya katikati ya wiki. Mbwana Samatta akiwa na KRC Genk ya Ubeligji wamefanikiwa kusonga mbele kwenye kombe la Ubelgji baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Cercle Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge usiku wa kuamkia jana. Katika mchezo huo Samatta alicheza dakika 75.

    Naye Mlinzi wa zamani wa Simba Abdi Banda akiwa na timu yake ya Baroka FC wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Banda alicheza dakika 90.

    Wakati huo Simon Msuva usiku wa juzi aliisaidia timu yake Difaa Hassan El-Jadida kusonga mbele katika Kombe la FA Morocco baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Ittihad Tanger Uwanja wa Grand Stade de Tanger. Msuva alicheza dakika zote 90 na kutoa mchango mkubwa kwenye ushindi huo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako