• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yawa klabu yenye mapato ya juu zaidi

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:40:48

    Klabu ya Manchester United imeripoti mapato ya pauni milioni 581 kwa kipindi cha fedha cha 2017 huku mapato ya televisheni yakiongezeka.

    Katika mwaka mmoja baada ya kushinda kombe la bara Yuropa, na EFL klabu hiyo imetia saini mikataba 12 ya ufadhili huku mapato ya matangazo pamoja na yale yanayopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.

    Klabu hiyo ilifaidika kutoka kwenye ongezeko la mapato ya televisheni wakati wa kipindi cha 2016-17 ikiwa ndio mwaka wa kwanza kati ya mitatu ya makubaliano ya matangazo ya TV.

    Tarehe 30 Juni mapato ya matangazo yaliongezeka hadi £194m kutoka £140m mwaka mmoja kabla ikiwa ni ongezeko la silimia 38. Msimu huu klabu hiyo imerudi katika ligi ya vilabu bingwa baada ya kushinda kombe la Yuropa dhidi ya Ajax mnamo mwezi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako