• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Borussia Dortmund aweka rikodi safi sana

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:41:17

    Ligi kuu nchini Ujerumani almaarufu kama Bundesliga inaendelea huku klabu ya Borussia Dortmund ikiendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo ya nchini humo. Bundesliga ni kati ya ligi ngumu ambayo makocha wakubwa kama Jurgen Klopp, Pep Gurdiola na Carlo Ancelotti wamepitia lakini hakuna aliyeweka rekodi ya Peter Bosz.

    Toka Bosz aichukue Dortmund wamekipiga na Wolfburg, Hamburger, Fc Colgne, Freiburg na Hertha BSC lakini hawajapoteza hata mchezo mmoja. Na kubwa zaidi timu yake imefanya ni kutoruhusu wavu wao kuguswa katika michezo hiyo. Peter Bosz anakuwa kocha wa kwanza katika historia ya Bundesliga kucheza michezo 5 katika ligi hiyo bila kuruhusu wavu wa timu yake kuguswa, jambo ambalo toka Bundesliga ianze hakuna aliyewahi kufanya.

    Peter Bosz msimu uliopita alikuwa kocha wa klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi ambapo alitua Borussia Dortmund kuchukua nafasi ya Thomas Tuchels aliyefungashiwa virago mwishoni mwa msimu uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako