• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan awataka wakazi wa Darfur wasalimishe silaha zao

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:55:20

    Rais Omar al Bashir wa Sudan amewataka wakazi wa jimbo la Darfur kusalimisha silaha zao kwa hiari kabla serikali haijaanza kunyang'anya silaha hizo kwa nguvu.

    Akiwahutubia watu mjini Nyala, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Darfur, Rais al-Bashir amesema amri ya watu kusalimisha silaha ni makini, na kusema silaha zinatakiwa kuwa mikononi mwa serikali tu na kutumika kwa ajili ya ulinzi na usalama wa wananchi na taifa. Hakuna takwimu rasmi kuhusu idadi ya silaha haramu katika jimbo la Darfur, lakini inakadiriwa kufikia milioni 2.

    Rais Al Bashir ambaye pia anafanya ziara katika jimbo la Darfur, amesema serikali yake inafanya juhudi kukomesha hali ya ukimbizi kwenye jimbo la Darfur, ambako wakimbizi wanapokea msaada wa makombo ya chakula na vitu vyenye sumu, hali ambayo amesema hailingani na desturi ya wasudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako