• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaadhimisha siku ya kimataifa ya amani kwa kutoa mwito wa umoja na amani

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:55:40

    Rwanda imeadhimisha siku ya kimataifa ya amani kwa kuhimiza umoja na masikilizano kati ya wanyarwanda na vizazi vijavyo.

    Maadhimisho hayo yalifanyika kwenye majengo ya bunge mjini Kigali, na kuhudhuriwa na maofisa wa serikali, vijana, watu kutoka taasisi zisizo za kiserikali na wasomi.

    Akiongea kwenye shughuli hiyo, mwenyekiti wa kamati ya umoja wa kitaifa na masikilizano ya Rwanda Bw John Rucyahana, amesema kiwango cha amani, umoja na masikilizano kilichofikiwa sasa, kinatakiwa kulindwa, ili Rwanda iweze kuwa na mustakbali mzuri zaidi.

    Hata hivyo Bw Rucyahana amesema kuna changamoto ambazo bado zinakwamisha umoja na masikilizano. Ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni watu kuendelea kujitambulisha kwa msingi wa ukabila, na itikadi ya mauaji ya halaiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako