• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakenya watoa mwito wa kuwepo kwa umoja na masameheano miaka minne baada ya shambulizi la Westgate

  (GMT+08:00) 2017-09-22 08:56:00

  Mke wa Rais wa Kenya Bibi Margaret Kenyatta ametoa mwito kwa wananchi kuungana na kusameheana wakati Kenya ikiwa kwenye kumbukumbu ya miaka minne tangu shambulizi la kigaidi la Westgate litokee na kusababisha vifo vya watu 67.

  Bibi Kenyatta aliyeongoza shughuli ya kumbukumbu hiyo, amesema kumbukumbu ya tukio hilo inaleta maumivu makubwa na masikitiko, lakini pia inawakumbusha wakenya kuungana kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.

  Amesema shambulizi la Westgate lilivuruga na kubadilisha maisha na ndoto za watu wengi, lakini pia ameonyesha imani yake kwa moyo wa wakenya kuunga mkono shughuli za kuwasaidia watu kama hao na jamii zilizoko hatari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako