• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe mkuu wa EU kwenye mazungumzo ya Brexit amshinikiza waziri mkuu wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2017-09-22 09:15:18

    Mjumbe mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit Bw Michel Barnier ameongeza shinikizo kwa waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa Mary May kwa kutaka Uingereza iweke bayana msimamo wake, ili kutoa mwelekeo kwa mazungumzo ya Brexit yaliyokwama.

    Bw Michel Barnier akitoa hotuba kwenye bunge la Italia amesisitiza kwamba mazungumzo ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya yanatakiwa kumalizika kabla ya tarehe 29 mwezi Machi mwaka 2019, miezi sita imeshapita tangu mazungumzo hayo yalipoanza, na miezi sita mingine itatumiwa kuthibitisha na kuidhinisha makubaliano yatakayofikiwa, hivyo bado imebaki miezi 12 tu kwa ajili ya mazungumzo.

    Amesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unapenda kufikia makubaliano na Uingereza. Lakini masuala kadhaa bado hayajatatuliwa, yakiwemo malipo ya Brexit, uhakikisho wa maslahi ya wananchi na upangaji wa mpaka wa Ireland Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako