• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq kushirikiana na Iran na Uturuki kukabiliana na kura za maoni jimbo la wakurd

    (GMT+08:00) 2017-09-22 09:15:37

    Wizara ya mambo ya nje ya Iran imetoa taarifa kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa Iraq, Iran na Uturuki wamekutana mjini New York na kutoa wito kwa jimbo la wakurd liache kupiga kura za maoni.

    Taarifa imesema nchi hizo tatu zitachukua hatua kwa pamoja kama jimbo la wakurd likiendelea na upigaji kura za maoni. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu wanaona kitendo cha jimbo la wakurd kupiga kura za maoni kinakiuka katiba ya Iraq, na kitaharibu mafanikio yaliyopatikana na Iraq kwenye opresheni za kijeshi dhidi ya Kundi la IS, hata kingeweza kuchochea mgogoro mpya usiodhibitika katika Mashariki ya Kati.

    Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa mazungumzo kati ya serikali kuu ya Iarq na serikali ya jimbo la wakurd, ndiyo njia sahihi pekee ya kutatua suala la jimbo la wakurd.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako