• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yathibitisha tarehe ya kurudia uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2017-09-22 09:28:07

    Tume ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC imetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa marudio utafanyika tarehe 26 Oktoba.

    Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa IEBC Bw Wafula Chebukati inasema ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata sheria, tume hiyo imeamua kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 17 Oktoba.

    Habari nyingine zinasema, rais Uhuru Kenyatta amesema uamuzi wa mahakama kuu ya Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti ulikuwa si wa haki, na mahakama kuu inatakiwa kutoa maelezo zaidi.

    Amesema athari na kipaumbele vilivyotolewa na hukumu hiyo, vinaonyesha kuwa majaji wanaweza kufuta uamuzi wa mamilioni ya wakenya bila kujali ushahidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako