• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kupeleka askari zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-09-22 09:36:07

    Wizara ya ulinzi ya Rwanda imesema, Rwanda itatuma askari 140 zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuunga mkono tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Rwanda inasema, kutokana na matakwa ya Umoja wa Mataifa, serikali ya Rwanda ilikubali kuongeza askari 140 kwenye batalioni ya askari ya miguu iliyowekwa huko Bangui.

    Majukumu ya kikosi cha kulinda amani cha Rwanda ni kulinda usalama wa sehemu mbalimbali za Bangui, hasa usalama wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na majengo muhimu ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako