• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WTO lapandisha makadirio kuhusu ongezeko la biashara ya dunia mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-09-22 09:36:41

    Kutokana na ongezeko la biashara barani Asia na ongezeko kubwa la uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, shirika la biashara duniani WTO limepandisha makadirio yake kuhusu ukuaji wa biashara ya dunia kwa mwaka huu hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 2.4 ya hapo awali.

    WTO imesema, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na ongezeko kubwa la uchumi wa nchi zinazofanya biashara zaidi hasa China, biashara ya dunia imeongezeka kwa asilimia 4.2 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

    Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa WTO Bw. Robert Azevedo amesema uchumi wa dunia bado unakabiliwa na matishio ya sera ya kujilinda kibiashara, hali ya kikanda kuzidi kuwa mbaya, na hasara kubwa za kiuchumi zinazotokana na maafa ya asili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako