• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MCL, KPMG zainua uchumi Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:55:39

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezipongeza kampuni za Mwananchi Communications Limited (MCL) na KPMG kwa kubuni na kuanzisha programu ya kuzishindanisha kampuni bora 100 za kati kwa ajili ya kuinua uchumi wa Taifa.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo, Mkuu wa huduma na elimu kwa Mlipakodi Bw Julius Mjenga amesema kubuni jambo hilo kunaleta tija kwa taifa na kuomba suala hilo liwe endelevu kwa sababu litaibua fursa nyingi ambazo zitaleta ushindani wa kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa. Aidha amewataka wafanyabiashara kuzingatia taratibu na kanuni za uendeshaji wa biashara hizo.

    Pia amesema wafanya biashara kufuata sheria kwa kulipa kodi na kuhakikisha kuwa wanadai risiti kama inavyotakiwa. Kwa upande wake, Mhariri Mkuu Mtendaji wa MCL Bakari Machumu amesema kuandaa programu hiyo ni kwenda sambamba na mabadiliko ya kiutendaji pamoja na kuunga mkono serikali katika uwajibikaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako