• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yaitaka TTCL iwe na ubunifu

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:56:04

    Serikali ya Tanzania imeitaka bodi mpya ya wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuacha kuremba, na kujikita kwenye ubunifu huku wakijielekeza kwenye ushindani dhidi ya kampuni zingine za mawasiliano nchini humo.

    Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha mapato makubwa yanatoka kwenye data. TTCL ambayo ilibaki nyuma kiushindani kwa muda mrefu, hivi sasa imeibuka kwa nguvu baada ya Serikali kuamua kuirejesha mikononi mwake kutoka kwenye ubia baina yake na Airtel.

    Hata hivyo, Profesa Mbarawa amesema hangependa kuona ikijivutavuta katika hali ya sasa ya soko la mawasiliano ambalo linahitaji ubunifu na mikakati mathubuti ili kuweza kumiliki soko.

    Naye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TTCL Omary Nundu amesema tangu ateuliwe wamefanya mambo mengi hadi sasa ikiwemo kuifufua kampuni hiyo, kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano pamoja na kuanzisha huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha maarufu kama TTCL Pesa.

    Mwaka 2016, TTCL ilipata Sh0.21 bilioni katika soko na mwaka huu wanatarajia kupata Sh0.3bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako