• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatetea kandarasi ya ujenzi wa barabara iliyobadhibiwa kampuni ya Marekani

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:56:24

    Serikali ya Kenya imesema mkataba wa ujenzi wa barabara ya kati ya Mombasa na Nairobi ya shilingi bilioni 300 iliyokabidhiwa kampuni ya Marekani ulifikiwa wakati wa ziara ya aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama mwaka wa 2015. Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ujenzi wa barabara nchini Kenya Bw Peter Mundinia amesema mkataba huo utaifanya Kenya kupokea ujuzi wa wamerekani wa ujenzi wa barabara.Mkuu huyo alikuwa akijibu taarifa kutoka kwa gazeti moja la Kenya lililodai kuwa kampuni hiyo ya Marekani Bechtel ilikabidhiwa tenda hiyo bila utaratibu kufuatwa.Wakati huo huo ubalozi wa Marekiani umetetea mkataba huo na kukemea madai kuwa ilitolewa baada ya Marekani kuunga mkono serikali ya jubilee kwenye uchaguzi.Barabara hiyo ya kilomita 473 utafadhiliwa kwa mkopo wa gharama ya chini na benki ya Exim nchini Marekani na OPIC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako