• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa UNAIDS aahidi kulinda upatikanaji wa dawa kama haki ya binadamu

    (GMT+08:00) 2017-09-22 18:12:53

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa Michel Sidibe ameahidi kutetea haki ya kibinadamu ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuwa na uwezo wa kupata dawa.

    Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Sidibe amesema jambo la muhimu ni ubora wa dawa, usawa, heshima, na upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kama haki ya binadamu. Pia amesema, makubaliano ya bei yakifikiwa yataharakisha upatikanaji wa dawa ya kizazi kipya ya kidonge kimoja kwa watu wanaoishi na UKIMWI katika zaidi ya nchi 90 zenye uchumi wa chini na wa kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako