• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la biashara huria la Shanghai lapata uzoefu mkubwa katika kuendeleza shughuli za biashara nchini China 

    (GMT+08:00) 2017-09-22 18:19:42

    Eneo la biashara huria la Shanghai ni eneo la majaribio ya biashara huria nchini China. Rais Xi Jinping alipotembelea eneo hilo mwaka 2014 alisema eneo hilo ni kama shamba kubwa la majaribio, baada ya kupata mavuno mazuri, linapaswa kueneza uzoefu wake kwa mashamba mengine. Katika miaka kadhaa iliyopita, eneo hilo limefanya majaribio na uvumbuzi mwingi, na kukamilisha utaratibu wa hali ya juu kuhusu uwekezaji na biashara ambao unakubaliwa na jumuiya ya kimataifa, pia limeeneza uzoefu wake kwa sehemu nyingine nchini China.

    Eneo la majaribio la biashara huria la Shanghai lilizinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka 2013. Katika siku kadhaa baadaye, mfumo wa "Dirisha moja" wa kuandikisha kampuni katika eneo hilo ulianzishwa. Mfumo huo ni uvumbuzi wa kwanza wa eneo la biashara huria la Shanghai. Mfanyakazi wa eneo hilo Wang Lianfeng anasema,

    "Kabla ya kuzinduliwa kwa eneo letu, mchakato wa kuandikisha kampuni ulikuwa unachukua muda awa siku 29 isipokuwa siku za mapumziko. Lakini sasa inachukua muda wa siku nne tu."

    Tangu lizinduliwe, eneo la biashara huria la Shanghai linatoa sera mpya karibu kila mwezi, sera hizo ni pamoja na kuzipa kampuni za nchi za nje hadhi kama kampuni za ndani isipo kuwa kama zipo kwenye sekta zinazopigwa marufuku kujishughulisha. Vilevile sekta kampuni za nchi za nje zinazopigwa marufuku kwa kampuni ya kigeni pia zinapungua hatua kwa hatua, hadi sasa sekta hizo zimebaki asilimia 5 tu kati ya sekta zote katika eneo hilo. Naibu mkurugenzi wa tume ya biashara ya serikali ya mji wa Shanghai Bw. Shen Weihua anasema,

    "Hatua hizo zimeleta ufanisi dhahiri. Hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu, eneo la biashara huria la Shanghai limeandikisha kampuni 7,860 za nchi za nje, ambazo zimewekeza vitega uchumi vyenye thamani ya dola bilioni 91.3 za kimarekani."

    Naibu mkurugenzi wa tume ya maendeleo na mageuzi ya mji wa Shanghai Bw. Zhu Min amesema eneo la biashara huria la Shanghai ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sehemu nyingine nchini China, na hadi sasa matokeo yake 23 katika uvumbuzi na mageuzi ya sera za fedha na biashara yameenezwa kote nchini.

    Mwezi Machi mwaka huu, baraza la serikali ya China lilitoa mpango wa kukuza zaidi mageuzi na kiwango cha ufunguaji mlango cha eneo la biashara huria la Shanghai, ambalo ni mpango wa tatu tangu liasisiwe. Bw. Zhu Min anasema,

    "Kwenye mpango huo, tumetetea sera kadhaa mpya, ambazo ni uvumbuzi wa kurahisisha shughuli za biashara, pia zinalingana na vigezo vya kimataifa vya ngazi ya juu zaidi. Tunalengea kuinua kiwango cha operesheni zetu kwa kuunganisha sera zetu na vigezo vya kimataifa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako