• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kenya zasaini makubaliano ya kuepusha kutoza ushuru kwa mara mbili

    (GMT+08:00) 2017-09-22 18:49:18

    Idara kuu ya ushuru ya taifa ya China na wizara ya fedha ya Kenya huko Nairobi zimesaini makubaliano ya kuepusha kutoza ushuru kwa mara mbili na kuzuia kukwepa ushuru kati ya serikali za nchi hizo mbili.

    Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema, utekelezaji wa makubaliano hayo unatarajiwa kuhimiza uwekezaji wa China nchini Kenya.

    Naye naibu mkurugenzi wa idara kuu ya ushuru ya China Bw. Sun Ruibiao amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kunaweza kupunguza mzigo wa ushuru wa walipaji, huku akitaka makubaliano hayo yaanze kutekelezwa mapema ili kutoa mchango katika uungaji mkono kwa ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako