• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria majadiliano ya mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-22 20:34:56

    Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria majadiliano ya mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alihudhuria majadiliano ya mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

    Katika majadiliano hayo, Bw. Wang Yi alisema, Umoja huo umetoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya binadamu, lakini bado haujatimiza ndoto ya binadamu wote kunufaika na amani, maendeleo na heshimu. Wang Yi amekumbushia wito uliotolewa na Rais Xi Jinping wa China katika majadiliano ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa miaka miwili iliyopita, aliposisitiza juu ya uhusiano mpya wa kimataifa uliokuwa na kiini cha kunufaishana katika ushirikiano, na kuunda jumuiya ya mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Bw. Wang Yi amesema China itaendelea kuleta manufaa makubwa zaidi ya amani, maendeleo na usimamizi, na itaunganisha ndoto yake na ndoto ya watu wote duniani, na kusaidia maendeleo ya pamoja ya nchi zote duniani. Pia amesema, China inapenda kushirikiana na nchi zote kutimia mustakabali mzuri wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako