• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Umoja wa Mataifa zasaini kumbukumu kuhusu pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja"

    (GMT+08:00) 2017-09-23 17:28:49

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana walihudhuria kwa pamoja sherehe ya utiaji sahihi wa "Kumbukumu ya maelewano kuhusu pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' kati ya Wizara ya mambo ya nje ya China na Idara ya mambo ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa" ambayo ilifanyika mjini New York, Marekani.

    Kumbukumbu hiyo inayohusisha sekta za ushirikiano wenye ufanisi, ujenzi wa uwezo, upashanaji wa uzoefu na utafiti kuhusu sera, inalenga kuhimiza pande hizo mbili kuimarisha ushirikiano, na kuzisaidia nchi zinazoendelea duniani ambazo zinajiunga na Pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" kuongeza uwezo wao wa kujiendeleza, kuhimiza ujenzi wa mradi huo na utekelezaji wa mipango ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Habari nyingine zinasema kuwa, katika mkutano wa mawaziri wa "kundi la nchi 77 na China", Bw. Guterres amepongeza umuhimu wa "kundi la nchi 77 na China" katika kuhimza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako