• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yasema kupiga kura za maoni ya raia kuhusu kujitenga eneo la wakurd na Iraq

    (GMT+08:00) 2017-09-23 18:06:53

    Ikulu ya Uturuki jana imetoa taarifa ikisema, upigaji wa kura za maoni ya raia kuhusu kujitenga eneo la waKurd na Iraq ambao utafanyika hivi karibuni utaleta matokeo mabaya.

    Taarifa hiyo inasema upigaji kura huo si halali, na kutatishia usalama wa Uturuki, amani na utulivu wa kanda hiyo, na ukamilifu wa ardhi ya Iraq.

    Taarifa hiyo imeitaka serikali ya eneo la Kurd nchini Iraq iondoe upigaji kura huo, na kutafuta njia ya usuluhishi chini ya mfumo wa katiba ya Iraq. Pia inasema Uturuki inapenda kufanya uratibu kati ya serikali ya eneo la Kurd na serikali kuu ya Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako