• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zataka msaada wa kimataifa katika juhudi za amani na usalama.

    (GMT+08:00) 2017-09-23 19:01:59

    Nchi za Afrika Ijumaa zimetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kutafuta amani na utoaji wa misaada ya kibinadamu katika kanda hiyo katika mkutano wa mwaka wa Baraza kuu la umoja wa mataifa.

    Rais wa Cameroon Paul Biya amesema amani bado ikohatarini kwa kutishiwa, hasa kutokana na ugaidi, mapambano, umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa na kuwa migogoro inayoendelea Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na mashariki ya kati, ambayo inaleta maumivu na shida. Amezitaka nchi zote za Afrika kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza amani.

    Naye rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera akielezea matumaini yake ya kutafuta amani na upatanisho kupitia mazungumzo.

    Mkutano huo uliofanyika jumanne umeshirikisha wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali za nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako