• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuajiri maafisa wa jeshi 3,000 ili kuimarisha jeshi hilo

    (GMT+08:00) 2017-09-24 18:19:35

    Rais wa Tanzania John Magufuli jana amesema Serikali itaajiri maofisa wa jeshi 3,000 ili kuboresha ufanisi wa huduma ya Jeshi la Ulinzi wa Tanzania (TPDF) nchini humo.

    Alitangaza ajira hizo mpya mjini Arusha kwenye sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maofisa 422 wa jeshi hilo. Amesema serikali ya Tanzania pia itatoa ajira 50,000 kwa watumishi wa umma mwaka huu, ongezeko hili la nafasi za ajira zinatokana na watumishi wasio na vyeti vinavyokubalika wanaoondolewa pamoja na hatua ya serikali ya kupunguza matumizi ya gharama, ambapo dola za kimarekani milioni 600.

    Magufuli amesisitiza juhudi za TPDF katika kudumisha amani na usalama nchini humo na katika operesheni kadhaa nje ya nchi.

    Tanzania kupitia TPDF inashiriki katika vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa Darfur Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Lebanon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako