• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yaomba kuimarisha amani kwa njia ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-09-24 18:20:07
    Sudan Kusini yaomba kuimarisha amani kwa njia ya maendeleo

    Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Bw. Taban Deng Gai ametoa wito wa kuhamasisha amani na utulivu kwa kuzingatia juhudi za maendeleo na miradi ya muda mrefu.

    Akiongea katika mjadala wa ngazi ya juu ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa, Sudan Kusini itaimarisha jitihada zake za kuboresha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, na kuongeza kuwa, nchi yake inatarajia jumuiya ya kimataifa itarekebisha njia ya kutoa msaada kwa mchakato wa maendeleo na mambo ya kibinadamu.

    Vile vile amesema lengo kuu ni kutoa nafasi ya amani kwa wananchi wote wa Sudan Kusini ili kuwawezesha kuchagua viongozi wao wenyewe kwa uchaguzi wa huru, wa haki na wa kuaminika na kuongeza kuwa, wameshuhudia wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao wakirejea nyumbani kwa hiari, na maendeleo yanayopatikana katika mazungumzo ya kitaifa.

    Tangu mwaka 2013, wakati mgogoro wa Sudan Kusini ulipotokea katika mji mkuu wa Juba, zaidi ya watu milioni mbili wa Sudan Kusini walikimbilia nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako