• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuepusha vita ya nyuklia na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:04:29

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steve Mnuchin amesema Marekani inataka kuepusha vita ya nyuklia na Korea Kaskazini. Akihojiwa na televisheni ya ABC News, Bw. Mnuchin amesema rais wa Marekani hataki vita ya nyuklia, na watafanya kila wawezalo kuepusha vita ya nyuklia. Bw. Mnuchin ni ofisa mwingine mwandamizi wa Marekani kutoa uhakikisho wa kutotaka vita ya nyuklia, baada ya rais Donald Trump wa nchi hiyo kutishia kuiangamiza Korea Kaskazini na serikali yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako