• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la mazingira la Tanzania kutoa vibali vya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:13:33

    Baraza la mazingira la Tanzania NEMC litaanza kutoa vibali kwa wawekezaji ndani ya siku tatu, ikiwa ni hatua ya kuhimiza maendeleo ya viwanda.

    Kaimu mkurugenzi wa baraza hilo Bw Vedasto Makota amesema kutolewa kwa vibali vya muda, kutaruhusu wawekezaji kuendelea na maandalizi ya uwekezaji kabla ya kuanza kwa uzalishaji.

    Bw Makota amesema kutolewa kwa vibali vya muda kutawasaidia wawekezaji kuepuka urasimu kwenye hatua za mwanzo za uwekezaji, na utaruhusu wawekezaji kuendelea na shughuli za uwekezaji huku NEMC ikiendelea na tathmini yake kuhusu madhara ya uwekezaji huo kwa mazingira.

    Kabla ya uamuzi huo wawekezaji kwenye shughuli za uzalishaji viwandani hawakuruhusiwa kuanza uzalishaji, kabla ya madhara ya shughuli zao kwa mazingira kufanyiwa tathmini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako