• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahandisi wa nchi za Afrika kujadili usimamizi wa taka wenye ufanisi

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:13:58

    Wahandisi wa nchi za Afrika wanakutana mjini Kigali kwenye mkutano wa pili wa wahandisi utakaofanyika kwa siku tano, kujadili usimamizi wenye ufanisi wa taka.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "usimamizi wa taka wenye ufanisi barani Afrika" unawakutanisha wajumbe 1,000 wenyeji, wa kikanda na wa kimataifa, ambao watajadili changamoto zinazohusiana na usimamizi wa taka, na kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa maendeleo endelevu ya usimamizi wa taka.

    Wakati mkutano huo unafanyika imefahamika kuwa asilimia 35.8 ya wanyarwanda wanatumia huduma ya utupaji taka, na asilimia 29 wanatupa vichakani karibu na makazi yao, na asilimia 0.2 wanachoma au kutupa mitoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako