• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaendelea kuwarejesha wakimbizi wa Somalia kutoka Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:35:18

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewarejesha wakimbizi 832 wa Somalia kutoka Kenya katika wiki mbili zilizopita.

    Kamishna mkuu wa shirika hilo amesema wakimbizi 83 walirudi mjini Mogadishu na wengine 749 walipelekwa mjini Kismayu, kusini mwa Somalia kati ya Septemba 1 hadi 15.

    Shirika hilo pia limesema jumla ya watu 71,034 walirejeshwa kwa hiari kutoka kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya.

    Serikali ya Kenya imesema hali ya wakimbizi inaendelea kutishia usalama wa Kenya na kanda hiyo mbali na msukosuko wa kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako