• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar yafanya juhudi kuziba pengo kati ya ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa uchumi

  (GMT+08:00) 2017-09-25 09:35:49

  Visiwa vya Zanzibar vinafanya juhudi za kupunguza pengo lililopo kati ya ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa uchumi.

  Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Bw. Khalid Salum amesema ongezeko la uchumi linatakiwa kufikia zaidi ya asilimia 10 ili kukabiliana na changamoto hiyo. Ameeleza kuwa ongezeko kubwa la idadi ya watu ni changamoto inayokwamisha maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.

  Ikilinganishwa na ongezeko la idadi ya watu katika Tanzania Bara ambalo ni asilimia 2.8, ongezeko hilo visiwani Zanzibar ni asilimia 3.1. Amesema ongezeko la idadi ya watu wa Zanzibar linazidi ongezeko la pato la Taifa, na Zanzibar inafanya juhudi za kupunguza pengo hilo.

  Takwimu zinaonyesha kuwa uchumi wa Zanzibar unaongezeka kwa asilimia 4.8 kila mwaka, ikilinganishwa na lengo la asilimia 5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako