• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wasiopungua saba wauawa katika mgogoro wa kikabila kaskazini magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:43:43

    Serikali ya Kenya jana imethibitisha kwamba watu wasiopungua saba wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mgogoro wa kikabila uliotokea usiku wa Jumamosi katika kaunti ya Narok, kaskazini magharibi mwa Kenya.

    Naibu kamishna wa kaunti hiyo Bw Mohammed Noor amethibitisha kwamba mapigano hayo kati ya wamaasai na wakipsigi yamelipuka baada ya uporaji ulioambatana na vurugu uliotokea katika eneo la Transmara Magharibi usiku wa Jumamosi.

    Amesema mfanyabiashara wa kabila la wamasai Ben Koleini akiwa ni mmoja wa wahanga wa tukio hilo, aliuawa na watu wenye silaha wasiojulikana wakati alipoanarudi nyumbani kwa gari lake katika eneo la Esoit. Mauaji hayo yalisababisha mauaji mengine ya kulipiza kisasi.

    Maofisa wa polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako