• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wapendekeza mpango mpya kuhusu amani Libya

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:48:48

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Bw. Ghassan Salame, amependekeza mpango mpya wa kutatua mgogoro wa kisiasa wa Libya katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Libya huko New York ulioongozwa na katibu mkuu wa umoja huo Bw. Antonio Gutterres.

    Mpango huo uliopendekezwa na Bw. Salame ni pamoja na marekebisho ya makubaliano ya kisiasa yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kufanya mkutano wa taifa unaoandaliwa na Umoja wa Mataifa kuyakutanisha makundi yote ya kisiasa ya Libya, kupitisha rasmi katiba na uchaguzi wa mwisho wa rais na wa bunge.

    Baadhi ya wabunge wa bunge lililoko mashariki ambao wanapinga makubaliano ya kisiasa ya hivi sasa, wamekaribisha pendekezo la Bw Salame, huku wengine wakilikataa.

    Mjumbe wa kamati ya mazungumzo ya bunge hilo Bw. Abdussalam Nasia amekaribisha mpango huo, akisema mpango huo ni pamoja na mwongozo wa kutatua mgogoro wa kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako