• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanasiasa aliyetaka kuwania urais nchini Rwanda akamatwa

  (GMT+08:00) 2017-09-25 18:13:22

  Mwanamke mmoja nchini Rwanda ambaye alitaka kuwania urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita nchini humo amekamatwa na polisi kwa tuhuma za makosa dhidi ya usalama wa taifa na udanganyifu.

  Taarifa iliyotolewa na polisi nchini Rwanda imesema, Diane Rwigara, ambaye ni mfanyabiashara, amekamatwa jumamosi iliyopita pamoja na mama yake na dada yake. Taarifa hiyo imesema, wakati upelelezi ukiendelea, polisi waligundua ushahidi dhahiri unaowahusisha watatu hao na uhalifu dhidhi ya usalam wa taifa.

  Uamuzi wa kuwakamata ulichangiwa na viendo vyao wakati wa uchunguzi wa awali, hususan kukataa kushirikiana na polisi na kutoa taarifa kwa umma ambazo, kisheria, zinatakiwa kuwa za siri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako