• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nusu fainali ligi ya mabingwa: Etoile du Sahel ya Tunisia yatinga nusu fainali.

    (GMT+08:00) 2017-09-26 08:45:01

    Klabu ya soka ya Etoile du Sahel ya Tunisia imekuwa timu ya mwisho kufuzu hatua ya nusu fainali michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa Al Ahli Tripoli ya Libya usiku wa kuamkia jana.

    Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa jijini Tripoli wiki iliyopita timu hizo zilitoka sare ya bila mabao hivyo Etoile imefuzu kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya ushindi wa jana.

    Timu zilizofuzu nusu fainali ni Wydad Casablanca ambayo itakutana na USM Alger wakati Al Ahly itacheza na Etoile du Sahel. Mechi za nusu fainali zitachezwa kati ya Septemba 29 na Oktoba 1 na kurudiwa kati ya Oktoba 20 na 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako