• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjadala wa wazi wa baraza kuu la 72 la Umoja wa Mataifa wafungwa

  (GMT+08:00) 2017-09-26 09:44:16

  Mjadala wa wazi wa Baraza kuu la awamu ya 72 la Umoja wa Mataifa umefungwa katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.

  Katika mjadala huo, wajumbe wa nchi mbalimbali wametoa maoni kuhusu kuimarisha ushirikiano, kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu na kukabiliana na tishio la kinyuklia, mabadiliko ya hali ya hewa, ugaidi na itikadi kali.

  Mwenyekiti wa baraza kuu la awamu 72 la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajčák ametoa hotuba akiihimiza tena jumuiya ya kimataifa kuimarisha mtazamo wa kutoa kipaumbele kwa maslahi ya binadamu. Amesema katika mjadala huo atatilia mkazo masuala muhimu ikiwemo kuzuia mapambano, kulinda haki za kibinadamu, kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw. Augustine Mahiga amesema, nchi hiyo inaunga mkono mageuzi yanayofanywa na Umoja wa Mataifa ambayo yanalenga kuufanya umoja huo kuwa na uhai zaidi katika kutatua changamoto zinazoikabili dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako