• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ADB yadumisha utabiri wa ukuaji wa uchumi wa China wa asilimi 6.7

    (GMT+08:00) 2017-09-26 18:04:49

    Benki ya Maendeleo ya Asia (ADB) imekadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa China utakuwa asilimia 6.7 kwa mwaka huu na asilimia 6.4 kwa mwaka ujao, ikiwa ni sawa na makadirio ya mwezi Julai ya Benki hiyo.

    Katika jarida la Mtazamo wa Maendeleo ya Asia mwaka 2017, ADB imesema mahitaji makubwa kutoka nje, sera nyumbufu za fedha, na manunuzi makubwa ya ndani yamesaidia kuchochea ukuaji nchini China.

    Uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 6.9 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, huku manunuzi na huduma, kwa pamoja na sekta mpya zinazochochewa na uvumbuzi zimechukua nafasi kubwa katika uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako