• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 4 katika robo ya pili ya 2017

    (GMT+08:00) 2017-09-26 19:03:51

    Uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 4 katika robo ya pili ya mwaka 2017 hasa ukisaidiwa na sekta ya kilimo na sekta ya huduma.

    Taakwimu za serikali zinaonyesha kwamba kati ya mwezi Aprili-Juni pato la kitaifa lilifikia franc 1,869.

    Hata hiuvyo katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ukuaji ulifikia asilimia 1.7 tu.

    Kwa jumla mwaka huu wa 2017 Rwanda inatarajia ukuaji wa kiuchumi wa asilimia 6.2.

    Sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 6 kwenye robo ya pili huku mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo yakiongezeka kwa asilimia 22.

    Nayo sekta ya huduma ilikua kwa asilimia 7 kutokana na utendaji mzuri wa hoteli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako