• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Biashara zafungwa kufuatia maandamano Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-26 19:05:25

    Biashara nyingi katika miji ya Nairobi na Kisumu nchini Kenya zimesalia kufungwa leo huku kufuatia maandamano ya kisiasa nchini humo.

    Wafanyabiashara walihofia kuporwa na waandamanaji waliokuwa kwenye eneo la katikati mwa mji mkuu Nairobi wakishinikiza kuondoka kwa mkurungezi mkuu wa tume ya Uchaguzi nchini humo Ezra Chiloba.

    Awali Rais Uhuru Kenyatta aliwaonya kuwa wale watakaopora au kutatiza biashara watachukuliwa hatua.

    Tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa utrais Septemba 1, shughuli za kibiashara nchini humo zimepungua huku soko la hisa likiwa na upungufu wa oparesheni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako