• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhifadhi wa mazingira waleta maendeleo endelevu ya utalii katika ziwa la Erhai

    (GMT+08:00) 2017-09-27 18:23:51

    Ziwa la Erhai lililoko mkoani Yunan kusini magharibi mwa China lililoko kwenye mwinuko wa mita 2,000 kutoka usawa wa bahari, linazungukwa na milima. Kando ya ziwa hilo lenye eneo la kilomita 256 za mraba, kuna miji na vijiji vingi, na kati yake mji wa Dali unajulikana zaidi kutokana na kuwa na mandhari nzuri na utamaduni maalumu wa makabila madogo madogo. Ili kupata maendeleo endelevu ya utalii, sehemu ya Erhai imefanya juhudi kubwa za kuhifadhi mazingira.

    Hivi karibuni kando ya ziwa la Erhai, kuna wakazi wa kudumu zaidi ya laki nane, mbali na hayo idadi ya watalii wanaotembelea sehemu hiyo inazidi milioni 10 kwa mwaka. Kutokana na shinikizo kubwa la matumizi ya maji, ziwa hilo zilikumbwa na maafa ya magugu maji mara mbili. Ili kuhifadhi mazingira, mwezi Machi mwaka huu, mji wa Dali ulichukua hatua nyingi ili kushughulikia uchafuzi wa maji. Katibu wa baraza la serikali ya mji wa Dali Bw. Zhang Yong amesema,

    "Mradi wetu wa kuzuia na kushughulikia uchafuzi kwenye maji unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwakani. Tunataka kutatua suala la uchafuzi wa mazingira kwanza, halafu tutatunga mpango wa maendeleo."

    Bw. He Licheng ana hoteli ndogo katika kijiji cha Gusheng cha mji wa Dali. Zamani alifanya kazi ya ufugaji wa samaki. Mwaka 2015 rais Xi Jinping wa China alitembelea kijiji hicho cha kabila la Wabai na kukifanya kijulikane kote nchini China, na kuleta watalii wengi kwa kijiji hicho. Hivyo Bw. He alianzisha hoteli ya kuwapokea wageni. Kwa kufuata wito wa serikali wa kuhifadhi mazingira, Bw. He alisimamisha hoteli yake ili kufanya marekebisho. Anasema,

    "Niliongeza dibwe moja ili kusafisha maji machafu kwa kutumia yuan 4,000. Baada ya kupita madibwe mawili, maji machafu yataingizwa mitambo maalumu ya kuyasafisha tena. Baada ya kufikia vigezo vya serikali, maji hayo yatasafishwa mara nyingine tena kwenye maboma ya serikali. Halafu yataruhusiwa kuingia ziwa la Erhai."

    tangu hatua za kushughulikia uchafuzi wa maji zianze kutekelezwa mwezi Machi mwaka huu, maji ya ziwa la Erhai yameboreshwa kidhahiri. Kutokana na mpango wa serikali, baada ya kumaliza mradi wa kuzuia na kushughulikia uchafuzi kwa maji, uandikishaji wa hoteli na mikahawa kando ya ziwa hilo utaidhinishwa na kupitishwa na serikali kwa kuchunguza hatua zao za kuhifadhi mazingira. Ofisa wa kijiji cha Gusheng Bw. He Qiaokun amesema ingawa serikali imeweka vigezo vikali, lakini wanakijiji wengi wana hamu ya kujishughulisha na utalii. Anasema,

    "Baada ya suala la uchafuzi kushughulikiwa, mazingira yetu yameboreshwa, na watu wanaishi maisha ya raha, huku watalii wanaotembelea kijiji chetu wakiwa na kumbukumbu nzuri zaidi."

    Mandhari nzuri na mazingira safi vinawavutia watalii wengi zaidi kutoka nchini China na nchi za nje, na kuwaletea watu faida zaidi. Hivi sasa kuhifadhi mazingira ni kipaumbele cha kijiji cha Gusheng, na pia ni mwamko kwa wanakijiji wote. Bw. He Licheng anaona kijiji chake kina mustakabali mzuri. Anasema,

    "Tulizaliwa hapa Erhai, tunatumai kuwa serikali itashirikiana na wakazi wote ili kuhifadhi mazingira ya Erhai. Kwani mazingira mazuri yatatuletea watalii wengi zaidi, na kutuwezesha kupata maisha bora zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako