• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuipiku Kenya katika ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2017-09-27 19:09:05

    Tanzania inakaribia kufanya kufuata nyayo za Ethiopia mwaka 2015 kwa kuipiku Kenya katika orodha ya nchi zinazoongoza kwa kiwango cha ukuaji uchumi miongoni mwa nchi za eneo la Afrika ya Mashariki.

    Kwa miaka mitano iliyopita, uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa asilimia saba, huku wa Kenya ukiongezeka kwa asilimia tano. Benki ya Dunia (WB) inakadiria kuwa, mwaka ujao uchumi wa Tanzania utashika nafasi ya tatu kwa kiwango cha ukuaji barani Afrika, nyuma ya Ethiopia na Ghana. Kwa mujibu wa WB, mwakani uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.2, Ghana asilimia 7.8 na Ethiopia utakuwa kwa asilimia 8.3. Hivi sasa Tanzania inashika nafasi ya tano miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

    Takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinaonesha kuwa miaka 20 iliyopita, uchumi wa Tanzania umeongezeka mara saba, lakini tangu mwaka 1997 uchumi wa Kenya umekua mara tano na huenda kwenye miaka ijayo hali itaendelea kuwa hivyo. Kwa mujibu wa takwimu hizo, kuna wakati uchumi wa Kenya ulikuwa mkubwa mara nne kuliko wa Uganda lakini pengo hilo sasa linapungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako