• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yajiunga na AfCoP

    (GMT+08:00) 2017-09-27 19:09:25

    Rwanda imejiunga na jukwaa la jamii ya Utendaji la Afrika (AfCoP),mpango wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao unawaleta pamoja wataalamu na serikali za bara la Afrika kujadili miundo ya kufikia usimamizi wa matokeo wa biashara,utawala,miongoni mwa mambo mengine.

    Hatua hii ya Rwanda inatajwa kuboresha usimamizi wa ujasiriamali na kuongeza ukuaji na kusaidia kuboresha maisha ya watu.

    Usimamizi wa matokeo ni pale ambapo watu na mashirika,ambayo yanachangia moja kwa moja katika juhudi za maendeleo,kuelewa michakato ya biashara zao,bidhaa na hudma,kuonyesha ni jinsi gani vinachangia katika matokeo yaliyolengwa.

    Kulingana na Meneja wa mradi wa AfCoP katiba benki ya AfDB Pierre Justin Kouka, jukwaa hilo linalenga kusaidia nchi wanachama na watu binafsi kujenga uwezo wa kusimamia biashara zao ili kufikia malengo yao ya maendeleo.

    Aliongeza kuwa benki hiyo inalenga kuhakikisha kwamba nchi wanchama zinakuwa miradi mizuri ambayo inasaidia kuboresha maisha ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako