• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Wawekezaji kutoka China kuwekeza katika sekta zausafiri wa majini na ujenzi

    (GMT+08:00) 2017-09-27 19:09:41

    Ujumbe wa wawekezaji kutoka China wako nchini Uganda kutathmini uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya usafiri wa majini na sekta ya ujenzi.

    Kulingana na Makamu wa Rais wa Uganda Edward Sekandi,miradi kama hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Uganda wakati ikijitahidi kufikia kiwango cha nchi ya uchumi wa kati.

    Rais wa kampuni ya CCCC Dredging (Group) Company Limited Kang Xuezeng alipokutana na makamu wa rais wa Uagnda alisema kampuni yao iko katika nchi 100 duniani kote.Alisema nchini Uganda wanajenga barabara kuu ya Entebbe na wanaangalia uwezekano wa kuwekeza katika usafiri wa majini katika ziwa victoria na sekta ya ujenzi.

    Aliongeza kuwa Uganda ni soko linaloibuka na wanashirikiana na serikali kujenga miundombinu jambao ambalo pia litatoa nafasi za ajira.

    Makamu wa Rais Edward Sekandi aliwahimiza wawekezaji kuwekeza katika sekta ya madini,utalii,miongoni mwa rasilimali nyenginezo za Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako