• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makocha wa kikapu wa chuo kikuu NCAA cha Marekani wakamatwa kwa rushwa

    (GMT+08:00) 2017-09-28 08:31:55

    Makocha wanne wa chuo kikuu cha mchezo wa Mpira wa Kikapu nchini Marekani 'NCAA' wamekamatwa kwa kosa la kuhusika na vitendo vya rushwa. Serikali ya Marekani imewakamata walimu hao pamoja na mtendaji mwandamizi kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Addidas akiwa ni miongoni mwa watu 10 waliyoshikiliwa na kushtakiwa.

    Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika la kipelelezi la 'FBI' chini ya Uratibu wa chama cha mchezo wa kikapu, waliokmatwa ni pamoja na makocha na wajumbe ambao wamekuwa wakiwapa mafunzo wachezaji wenye vipaji zaidi kuhudhuria mafunzo katika vyuo vingine. Makocha hao wa 'NCAA' ni kocha msaidizi wa Chuo kikuu cha Taifa cha Oklahoma, Lamont Evans, kocha msaidizi wa Chuo kikuu cha Auburn, Chuck Person, kocha msaidizi wa Chuo kikuu cha Arizona, Emanuel "Book" Richardson na Tony Bland ambaye ni kocha msaidizi wa Chuo kikuu cha Southern California.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako