• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • West Ham na Tottenham zaadhibiwa na chama cha soka 'FA'

    (GMT+08:00) 2017-09-28 08:33:33

    Klabu ya West Ham na Tottenham za nchini Uingereza zimeadhibiwa na chama cha soka 'FA' kwa kitendo cha wachezaji wao kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wao wa derby uliyowakutanisha wababe hao siku ya Jumamosi katika jiji la London. Katika mchezo huo ambao uligubikwa na vurugu dakika ya 95 kwa baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili kutoelewana baada ya muamuzi, Michael Oliver kuipatia Spurs 'free-kick' kutokana na makosa yaliyojitokeza kwa mchezaji wa West Ham, Andy Carroll dhidi ya Fernando Llorente.

    Wachezaji, Carroll, Llorente, Winston Reid na Eric Dier wamehusishwa katika vurugu hizo na hivyo timu zao zitapaswa kuwa na majibu yakueleza mbele ya FA. Klabu hizo sasa leo zitatakiwa kujibu mashtaka yanayowakabili. Katika mchezo huo Spurs iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako