• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muingereza Kyle Edmund atolewa katika raundi ya pili ya michuano ya wazi ya Chengdu

    (GMT+08:00) 2017-09-28 08:33:57

    Mchezaji tenis muingereza, Kyle Edmund ambaye anashika nafasi ya 46 katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani ameondolewa na Mmarekani Jared Donaldson katika michuano ya wazi ya Chengdu 'Chengdu Open' ya hapa China yakiwa katika raundi ya pili. Edmund amefungwa kwa seti 6-0 1-6 6-4 na Donaldson ambaye anashikilia namba 58 kwenye viwango vya ubora vya tenisi duniani. Katika raundi ya kwanza Edmund, 22, ameibuka na ushindi dhidi ya Bernard Tomic katika michuano hiyo ya wazi ya Chengdu lakini alinyamazishwa na Donaldson, 20, katika seti ya tatu.

    Katika michezo mingine iliyopigwa jana Jumatano muhispania Albert Ramos alikipiga dhidi ya Lajovic, Julio Peralta dhidi ya Michael Venus huku Peter Gojozyk akikipiga na Leonardo Mayer.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako