• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha Andre Agassi kuendelea na kibarua cha kumfunza Novak Djokovic hadi mwaka 2018.

    (GMT+08:00) 2017-09-28 08:34:41

    Timu ya mchezaji tenis maarufu duniani, Novak Djokovic imethibitisha kuwa kocha Andre Agassi ataendelea na kibarua hicho hadi mwaka 2018. Bingwa mara 12 wa taji la Grand Slam, Djokovic alimuweka, Agassi katika timu yake mwezi May kabla ya kuanza kwa michuano ya wazi ya Ufaransa 'French Open' na kufanyakazi pamoja kwa miezi miwili sasa.

    Baada ya michuano ya Wimbledon, kulikuwa na uvumi kuwa kocha huyo raia wa Marekani angeendelea na kibarua chake cha kumnoa msebia, Djokovic ambaye aliishia hatua ya robo fainali ya mashindano ya wazi ya Ufaransa na yale ya Wimbledon huku akishinda ya Eastbourne baada ya miezi sita.

    Novak Djokovic anatarajia kurudi tena katika michuano ya wazi ya Australia 'Australian Open' mwezi Januari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako