• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaonyesha vitabu kuhusu magonjwa ya kitropiki, na uchapaji wa kale kwenye maonyesho ya vitabu Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-09-28 09:28:42

    Ujumbe wa sekta ya uchapishaji ya China jana ulifanya maonyesho ya vitabu vinavyoeleza namna ya kuzuia na kutibu magonjwa ya kitropiki, kwenye maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya siku tano yaliyofunguliwa huko Nairobi.

    Maonyesho hayo yanayoandaliwa na idara ya uchapaji ya Kenya, yanavutia washiriki mbalimbali wa riwaya na vitabu vya mambo halisi.

    Mjumbe wa China kwenye maonyesho hayo Bw Chen Yingjie amesema maonyesho hayo yanafahamika sana nchini China, na wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya maonyesho hayo.

    Bw Chen amesema ushirikiano kwenye mambo ya fasihi kati ya China na Kenya ni moja ya njia za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako