• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Mali za maduka ya jumla ya Nakumatt kupigwa mnada wiki ijayo

    (GMT+08:00) 2017-09-28 18:44:22

    Mali ya duka la jumla la Nakumatt itawekwa mnadani wiki ijayo ili kulipa deni la shilingi 180 inayodaiwa na halmashauri ya ushuru ya Uganda.

    Amri hiyo imetolewa na tume ya ushuru baada ya uamuzi wa mahakama kuitangaza Nakumatt kufilisika rasmi.

    Mali za duka hilo zitauzwa kwa umma kupitia mnada pamoja na kuuziwa watu binafsi.

    Hata hivyo,iwapo usimamizi wa maduka hayo ya jumla utaamua kulipa madeni wanayodaiwa mnada huo utasitishwa kabla ya tarehe ya mnada.

    Maduka ya jumla ya Nakumatt yanakabiliwa na wakati mgumu wa biashara kufuatia hasara kubwa walizopata.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako