• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:biashara ya samaki yashuka.

    (GMT+08:00) 2017-09-28 18:45:18

    Licha ya serikali ya Kenya kuwekeza fedha nyingi katika biashara ya ufugaji samaki ,mapato ya biashara hiyo yamepungua kwa kiasi kikubwa.

    Kiwanda cha samaki cha Wamagana kilichojengwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 61ili kuhimiza kilimo cha ufugaji wa samaki katika eneo la Nyeri kinakumbwa na ukosefu wa fedha kufuatia wateja wachache wa samaki.

    Rose Kariuki ,afisa katika kiwanda hicho amesema idadi ya wateja wanaonunua samaki hao iko chini ya matarajio .

    Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji samaki Charles Mbaoni amesema licha ya changamoto wanazozikabili kuhakikisha wanapata samaki wa kutosheleza soko,idadi ya wateja wa samaki Kenya iko chini ikilinganishwa na nchi za Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako