• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Carlo Ancelotti atimuliwa katika klabu ya Bayern Munich

    (GMT+08:00) 2017-09-29 08:40:18

    Carlo Ancelotti amefukuzwa kazi katika klabu ya Bayern Munich. Kufuatia kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya PSG, bodi ya klabu hiyo iliamua kumtimua raia huyo wa Italia ambaye alichukua nafasi ya Pepe Guardiola msimu uliopita.

    Ancelotti mwenye umri wa miaka 58, aliisaidia Bayern kushinda taji la Bundesliga, lakini hawakuweza kufika katika raundi ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa pamoja na nusu fainali ya kombe la Ujerumani.

    Naibu meneja Willy Sagnol ataiongoza klabu hiyo kwa muda. Bayern wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, wakiwa alama tatu nyuma ya Borussia Dortmund, na wakiwa wameshinda mara nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako